Sokwe wa Michael Jackson atimiza miaka 42

Sokwe wa Michael Jackson atimiza miaka 42

Sokwe wa aliyekuwa mfalme wa pop Michael Jackson ametimiza miaka 42 tangu kuzaliwa kwake.

Sokwe huyo aitwaye Bubble ambaye kwa sasa anaishi katika hifadhi maarufu huko Florida enzi za uhai wa MJ, alisafiri nae kimataifa na kushiriki katika ziara tofauti tofauti za mwimbaji huyo.

Kupitia chapisho lililowekwa na hifadhi hiyo la kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa sokwe huyo wamesema ni miongoni mwa sokwe maarufu katika hifadhi hiyo na tangu awasili hapo amenawili sana.

Bubble amewahi kuwa sokwe maarufu duniani kwa kuonekana kwenye video mbalimbali za muziki, ziara za kimataifa, pamoja na vipindi vya Television lakini kwa sasa amekuwa akionesha uwezo wake wa kuchora katika hifadhi hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags