Kim na kanye kwenye vita mpya kisa P Diddy

Kim na kanye kwenye vita mpya kisa P Diddy

Rapa na mtayarishaji tokea Marekani, Kanye West anaripotiwa kuingia kwenye vita mpya na aliyekuwa mke wake mwanamitindo, Kim Kardashian kufutia rapa huyo kumshirikisha binti yao North West kwenye wimbo wake mpya akiwa na P Diddy.

Machi 15 Kanye aliachia kionjo cha wimbo huo unaoenda kama 'Lonely Roads Still Go To Sunshine' ukiwajumuisha Diddy na mwanaye Christian Combs, na North akirap "When you see me shining, then you see the light."

Kim anadaiwa kujaribu kuzuia wimbo huo kutoka kwa hatua za kisheria, akituma barua za onyo na kutafuta msaada wa mahakama.

Hata hivyo kuna baadhi ya jumbe zimevuja kwenye mitandao ya kijamii zikimeonyesha Kanye akimtishia Kim kwa kuhusu North, huku Kim akisisitiza anamlinda binti yao.

Aidha, Vita hii inakuja ikiwa ni wiki moja baada ya Kanye kutangaza anaifufua ibada yake ya jumapili 'Sunday Service', ambapo waimbaji wote wakiwemo watoto watalazimika kunyoa vichwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags