Kama ilivyo kwenye mpira wa miguu ni sifa kwa mchezaji kucheza miguu yote kulia na kushoto. Hata kwenye muziki ni hivyo. Mtayarishaji anayeweza kuimba, kuandaa biti na melodies au msanii anayeweza kuimba na kutayarisha biti pia huonekana bora zaidi. kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kuna wasanii wamebarikiwa vipaji vyote hivyo kuimba, kuandaa melodies na kutayarisha muziki baadhi yao ni hawa.
S2kizzy, huyu ni moja ya watayarishaji wanaotajwa kuwa bora zaidi kwa sasa kutokana na uwezo wake wa kutengeza ngoma hit . Uwezo wake haujaishia kwenye kuanda ngoma kali tu bali hushiriki kwenye kuandika, kuimba na kuandaa melodies za nyimbo kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Ameshiriki kuimba katika nyimbo kama Dogoli ya kwake Country Wizzy, Gibela ya Chino Kidd ft Rayvanny & Mfana Kah Gogo, Pochi Nene ya Rayvanny, Hesabu ya Nikki Wa Pili ft Joh Makini, Haya ya Country Wizzy ft Khaligraph Jones. Katika ngoma zote hizo ameshiriki katika kuandaa biti na kuimba kiitikio pamoja na verse lakini pia kuandaa melodies.
Mr. T-Touch, ni mtayarishaji ambaye hajaishia tu kuandaa biti kwa wasanii pekee bali amewahi kushiriki katika uimbaji wa nyimbo za wasanii mbalimbali kama vile. Hatuna Ratiba ambayo yupo na Rapcha, Billnass, Chibau na Cheq Bob pia ameshiriki katika kuandaa na kuimba kiitikio kwenye ngoma ya Mr. Boniventure ya kwake Stamina.
Mwaka mmoja uliyopita Touch alishirikiana na Platform kwenye ngoma ya Dawa, Mwanzo Mwisho akiwa na Moni Centrozone, miaka nane iliyopita alishirikishwa na Professor Jay katika ngoma yake ya Pagamisa na ngoma nyingine nyingi.
Ukiachilia mbali Touch kushiriki katika ngoma hizo amefanikiwa pia kutengeneza hit kama mtayarishaji.
Abbah Process, akiwa kama mmoja ya watayarishaji mahiri wa muziki nchini kwa sasa, ameshiriki kuimba katika baadhi ya nyimbo ambazo ni pamoja na Gari Yangu akiwa na Young Dee, Chibonge akiwa na Marioo, G Nako, Byter Beast. Hata hivyo Abbah amewahi kuachia album yake inayoenda kama ABBAH THE EVOLUTION ambayo ilitoka mwaka 2021 akiwashirikisha wasanii wenye majina makubwa nchini akiwemo Jux, Harmonize, Marioo, Darassa na wengine.
Mocco Genius, ambaye ni mtayarishaji lakini pia ameonesha mapenzi yake katika muziki wa Bongo Fleva kwa kushiriki kuimba na kutengeneza ngoma kali kama vile Nikupe (2025) Sina (2024), My Love (2024), Mimi (2024), Mar Gaya (2024), Mchuchu feat. Alikiba (2024), Hello (2024), Mi Nawe feat. Marioo (2023), Yamenishika (Remix) feat. Nandy (2023), Nikilala (2023), Niheme (2022), Napendwa Remix ft. Alikiba, Fitingi feat Marioo (2025).
Genius Jini X66, huyu ni mtayarishaji ambaye mara nyingi anafanya kazi na Jay Melody na kila wakutanapo hutengeza ngoma kali na hit mfano wa ngoma hizo ni pamoja na Nakupenda ambayo imeandika rekodi kubwa kwenye historia ya muziki wa Bongo Fleva, Far Away na nyingine nyingi.
Pamoja na kutengeza hit pia ameshiriki kwenye uimbaji wa nyimbo kama Far Away ambayo amemshirikisha Jay Melody, My Chunun ya Cliv, Juu ya Jay Melody, Wewe feat Jay Melody, Kamtu na nyingine nyingi.

Leave a Reply