Beyonce, Jayz watajwa mashuhuda kesi mpya ya Diddy

Beyonce, Jayz watajwa mashuhuda kesi mpya ya Diddy

Rapa Sean 'Diddy' Combs anakabiliwa na mashtaka mapya ya biashara ya kuuza binadamu na unyanyasaji wa kingono baada ya Joseph Manzaro kudai alifanyiwa unyanyasaji na rapa huyo mbele ya mastaa wengine.

Manzaro ambaye ni mwenyeji wa Florida amesema alinyanyaswa kingono na Diddy katika moja ya party zake iliyofanyika Aprili 2015. Ambapo mastaa wengi walishuhudia akiwemo Beyonce, Jay Z, LeBron James na Gloria Estefan.

Manzaro anadai aliwekewa madawa kwenye kinywaji chake na Emilio pamoja na Gloria Estefan baada ya kushtuka alijikuta yupo kwenye kisiwa cha 'Star Island' Miami.
Anasema kwamba Lebron James alimuona na badala ya kumpa msaada akamuambia "Ni bora kufanya kitu kuhusu hilo."

Manzaro anadai alipitishwa kwenye njia za siri hadi kwenye nyumba ya Diddy na mshitakiwa Adria English, ambao anadai alikutana na Beyonce na Jay Z. anadai alivalishwa nguo za kike na kisha akaanza kucheza mbele ya watu.

"Beyonce, Jay Z na Lebron James walikuwepo wakati Diddy ananidhalilisha" amesema Joseph Manzaro

Hata hivyo, timu ya wanasheria wa Diddy imekanusha shtaka hili kwa kusema ni uongo na mlalamikaji anatafuta malipo kutoka kwa mshatikiwa.

"Malalamiko haya yanaonyesha urefu wa upotovu wa walalamikaji wanaopambana na vichwa vya habari, katika kutafuta siku ya malipo. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayesoma malalamiko haya huu ni uongo mtupu na asitarajie chochote," wamesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags