Diddy Kuvaa Mavazi Ya Kiraia Wakati Wa Kesi Kusikilizwa

Diddy Kuvaa Mavazi Ya Kiraia Wakati Wa Kesi Kusikilizwa

Sean "Diddy" Combs, ambaye anakabiliwa na mashtaka mazito ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono na uhalifu mwingine, amepata ruhusa ya kuvaa mavazi ya kiraia wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake inayotarajiwa kuanza Mei 5, 2025.

Uamuzi huu umetolewa na Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Kusini mwa New York, Arun Subramanian baada ya kupokea ombi kutoka kwa timu ya wanasheria wa Combs. Huku ruksa hio ikitolewa kwa lengo la mtuhumiwa huyo kutotafsiriwa vibaya akiwa na mavazi ya gerezani.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Combs ataruhusiwa kuwa na mashati matano ya mikono mirefu, suruali tano, sweta tano, soksi tano, na pea mbili za viatu visivyo na kamba vitu ambavyo atavitumia wakati wa kesi yake kusikilizwa.

Combs, ambaye amekuwa kizuizini katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn tangu Septemba 2024, anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, uhalifu wa kupanga (racketeering), na makosa mengine yanayohusiana na unyanyasaji wa kijinsia.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa endapo mwanamuziki huyo atapatikana na hatia basi atatumikia kifungo cha maisha jela.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags