Bill Gates: Miaka 10 Ijayo Binadamu Kufanya Kazi Siku Mbili

Bill Gates: Miaka 10 Ijayo Binadamu Kufanya Kazi Siku Mbili

Mmoja wa matajiri zaidi duniani na mfanyabiashara Bill Gates ameeleza kuwa miaka 10 ijayo binadamu watafanya kazi siku mbili kwa wiki huku majukumu yao yakifanywa na Akili Bandia (AI), hali itakayofanya siku zilizobaki kuwa muda wa mapumziko.

Ameeleza kuwa jamii italazimika kufikiria upya jinsi ya kutumia muda huo mpya wa ziada, akibainisha kuwa AI inaweza kutoa huduma za madaktari na walimu wa kuaminika, jambo ambalo linaweza kumaliza uhaba katika sekta ya afya na elimu.

Gates anaelezea mabadiliko haya kama fursa ya neema na wingi, ambapo roboti zinazoendeshwa na AI zitashughulikia hata kazi za mikono, na kuwaachia watu nafasi ya kubuni vitu vipya na kuenjoy maisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags