Wakati watu wakitulia kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani, upande wa burudani umezua gumzo zito baada ya mwanamuziki Diamond Platnumz kushiriki picha akiwa na mpenzi wake Zuchu, licha ya wawili hao kudaiwa kuwa tayari waliachana.
Kitendo hicho kimewaacha mashabiki na maswali mengi, huku wengi wakijiuliza kuhusu hali halisi ya uhusiano wao.
Kwa muda mrefu, kumekuwepo na tetesi kuwa Diamond Platnumz na Zuchu hawapo tena katika mahusiano, huku tukio la Zuchu kutoonekana kwenye harusi ya Jux na Priscilla nchini Nigeria likionekana kuchochea zaidi uvumi huo. Hata hivyo, sasa inaonekana tetesi hizo zimepata majibu, baada ya wawili hao kushiriki video na picha wakiwa pamoja katika hali ya kimahaba.
Baada ya kuonekana pamoja na kuzima kabisa uvumi wa kuachana, mashabiki wamejaa furaha huku wakimiminika kwenye mitandao ya kijamii kutoa komenti za pongezi, wengi wakifurahia kuona wawili hao wakiwa bado wapo pamoja.
“Tukiachana na chuki zinazopandikizwa Kwa zuchu ila uyu binti ni mzuri na wameendana bwana ake wallah ndo hivyo watu kumuandama Wallah,” “Ila mapenzi, ndomana siingiliagi ugomvi wa mahusiano ya watu. Wameendana wenyewe,” , “Midomo yote imefungwa 😂😂😂😂😂😂 kwani yule mbwa ni nani namtafuta ujueee😂😂😂😂🙌,”
“Hee , wapendanao wakigombana shika jembe ukalime 😂🙌🙌,” ” Haya mahusiano wafike mwisho wajali kilimo, mambo yao nasio haya mahusiano diamond anajua anachokifanya na zuchu kwa sasa mwache kuwaongelea haina maana kuwa pamoja au kuwachana wataamua wao mahusiano ni ya watu wawili kama awajaamua basi msiwaongele zuchu kaamua kupenda anachotaka,”
Huku wengine wakiandika “Mtangoja sana zuchu kuachika kwa simbaaa😂😂😂😂 dj niwekee nyimbo ya simba mtasubiri sanaaaaa, mbona bado na presha zitawashuka na kupandaaaaa,”,
“Ila Zuchu na Dai wanachanganya watu bhana anyway ni good sana mpaka wabishane na kupigana wenyewe wanaenjoy tu,” “Wambea mko wapi, haha haha haha haha, mtachoka, simwachane na mapenzi ya watu, mnaandika Kila siku zuchu zuchu zuchu, wanaume wote wako hivo kwani ni diamond peke,”.

Leave a Reply