Miaka 25 Kwa Rema Imetosha Kuonesha Ukubwa Wake

Miaka 25 Kwa Rema Imetosha Kuonesha Ukubwa Wake

Divine Ikubor, maarufu kama Rema, ni miongoni mwa wasanii wachache wa kizazi kipya waliothibitisha kuwa umri si kikwazo cha mafanikio. Licha ya kuwa bado kijana, Rema ameendelea kuwapa somo la muziki hata magwiji waliotangulia katika tasnia, kupitia mafanikio yake ya kipekee ambayo baadhi ya mastaa hawakuwahi kuyafikia.

Akitimiza miaka 25, Rema ambaye amezaliwa Mei Mosi, umri wake umetosha kabisa kuonesha ni kwa namna gani anaweza kufamnya makubwa zaidi katika tasnia ya burudani pamoja na kuupeleka muziki wa Afrobeat kimataifa zaidi.

Haya Ndio Mafanikio Yake Makubwa Kwenye Gemu Ya Muziki.

Wimbo "Calm Down" (feat. Selena Gomez) kufanikiwa Kimataifa

Baada ya kuachia ngoma "Calm Down" mwezi Februari 2022, Rema alipokea mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki duniani kote. Umaarufu wa wimbo huo ulimfungulia milango ya kushirikiana na mwanamuziki nyota wa Marekani, Selena Gomez, na kuifanya ngoma hiyo kuwa maarufu zaidi kimataifa.

Remix ya “Calm Down” kati ya Rema na Selena Gomez iliufanya wimbo huo kuwa mojawapo ya nyimbo za Afrobeats zilizofanikiwa zaidi duniani. Remix hiyo ilifanikiwa kufikisha zaidi ya watuazamaji bilioni 1 kwenye mtandao wa YouTube, jambo ambalo ni nadra sana kwa wasanii wa Kiafrika.

Aidha, wimbo huo uliingia kwenye chati maarufu ya Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya tatu, mafanikio ambayo yalimweka Rema katika historia kama msanii wa kwanza kutoka Afrika kufikia mafanikio hayo.

Tuzo ya MTV Europe Music Awards (EMAs)
Licha ya kufikisha watazamaji zaidi ya Bilioni 1 Rema, alinyakuwa tuzo ya Best Afrobeats katika MTV Europe Music Awards (EMAs) mwaka 2023, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kipengele cha Best Afrobeats kuanzishwa katika historia ya tuzo hizo, huku ushindi huo ukiashiria hatua kubwa katika muziki wa Afrobeats kimataifa.

Albamu Yake "Rave & Roses"
Akiwa na umri mdogo kabisa msanii huyo aliachia album yake ya kwanza iitwayo Rave & Roses, ilitoka mwaka 2022, albumu hiyo iliweka rekodi kwa kuwa albamu ya Afrobeats ya kwanza kufikisha milioni 1 za streams kwa siku moja kwenye Spotify. Albamu hio ilimuweka Rema kama msanii wa kimataifa, si tu wa Nigeria.

Ikumbukwe Rema alianza kuimba mwaka 2019 wimbo wake wa kwanza ukiwa ni "Dumebi", uliotoka Machi 2019 ngoma ambayo ilisimamiwa na lebo ya Jonzing World kwa ushirikiano na Mavin Records.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags