Diamond kuzipamba Tuzo za CAF 2024

Diamond kuzipamba Tuzo za CAF 2024

Mwanamuziki Diamond Platnumz amechaguliwa na Shirikisho la Mpira Afrika CAF kuwa msanii kinara atakaye tumbuiza kwenye shereshehe za ugawaji wa tuzo za CAF 2024 zitakazofanyika Jumatatu Desemba 16, 2024 katika Ukumbi wa Palais des Congres nchini Morocco.

Mbali na ugawaji wa tuzo, pia kutakuwa na mastaa wa muziki ili kuvutia mashabiki watakaokuwa wakitazama duniani kote. Diamond atachangia jukwaa hilo na wasanii wengine kama Dystinct, mwimbaji kutokea nchini Morocco anayesifika kwa kuchanganya mtindo wa R&B, Afrobeat na Kiarabu katika muziki wake.

Pia kutakuwa na maonyesho kutoka kwa kikundi cha Okestra Trio Andalou, kikundi cha wanawake cha 'Women in Jazz' na onyesho la ngoma lililoandaliwa na Adil Nakach, dancer wa Hip-Hop na House kutoka Casablanca.

Tuzo za CAF za 2024 zitaangazia wachezaji, makocha na timu bora zaidi barani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags