Point of no Return ni filamu, kuna pisi kali ilionekana humo. Ina sauti laini na mvuto wa asili uliovutia wengi. Kubwa zaidi ni ubora wake katika kutendea haki 'sini' na 'skripti'.
Japo ilikuwa filamu ya kwanza kwake. Alionesha uwezo wa juu. Waliotazama bila shaka walikiri, kwamba sanaa yetu imepata staa haswa. Muite Wema Sepetu.
Kuanzia hapo Wema hakutajwa kama Miss Tanzania wa skendo nyingi. Alitajwa kama staa wa filamu mwenye mvuto. Baada ya filamu hiyo na kadhaa, kila kitu 'kilichenji'
Kwenye sanaa kuna 'chenjizi' na kwa Wema kuna 'chenjizi' pia. Hatumtaji kwa ubora wa filamu. Hayupo tena kifilamu kama yule wa zamani. Japo anatamba na ‘taito’ ya staa wa filamu.
Ukitaja wasanii bora, watakaotaja jina la Wema kwa sasa hata kama wapo. Lakini kwa filamu ipi sasa? Labda atasimama na filamu zile za kale, ila kwa sasa ‘krauni’ ipo kwa wengine.
Inawezekana baada ya filamu ya 'supastaa' kutamba magazetini zaidi, kuliko ukweli halisi aliona inatosha. Wema aamke alipo sasa na kufanya vitu kwa ajili ya kipaji chake. Uwezo huo upo.
Ana jina kubwa, ila halijajengwa kupitia filamu. Msingi wa jina la kifilamu ulianguka. Natamani sana kumuona Wema akionesha ubora kama ule wa mwanzoni. Sijui itatokea lini?
Leave a Reply