Vitu vitano alivyowahi kufanya Rais Obama viliyomuonesha kuwa sio Rais wa kawaida

Vitu vitano alivyowahi kufanya Rais Obama viliyomuonesha kuwa sio Rais wa kawaida

Wengi wanamjua Rais Barack Obama kama Rais wa kwanza mweusi wa nchi ya Marekani. Vilevile, Rais huyo anajulikana kati ya maRais wacheshi, wachangamfu, mwenye upendo, yaani in short alikuwa "Cool President."



WaTanzania wengi pia wanapenda zaidi kumfananisha Rais Obama na Rais wa awamu ya nne Tanzania, Rais Kikwete, ambapo hata hivyo kuna kipindi wawili hao walikutana hapa nchini baada ya Rais Obama kuja kutembelea Tanzania.

 

Leo ninakuletea vitu vitano ambavyo Rais huyu kipenzi cha watu amewahi kuvifanya akiwa madarakani ambavyo vinaonesha ni namna gani yeye alikuwa ni rais wa kipekee na mwenye kupendwa haswa, haya twende kazi:

1. THE BEER SUMMIT (Obama anywa bia na wapinzani)



Rais Obama aliandaa mkutano na Henrt Louis Gates Jr, Mmarekani mweusi ambaye ni Professor wa chuo cha Havard pamoja na polisi wenye rangi ya kizungu katika nyumba yake, baada ya kuwa na mzozo mkubwa ambapo Gates alikamatwa nje ya nyumba yake na polisi huyo kutokana na mtu kuripoti polisi juu ya kuvamiwa nyumbani kwake. Obama alisema kuwa polisi waliact kijinga, jambo lililongeza mzozo zaidi.

Obama alifanya hivyo ili kuwakutanisha pande zote mbili na kutatua tatizo lao ambalo wengi waliliona kama ubaguzi wa rangi. Mkutano huo uliofanyika White House ulikuwa ni wa kunywa bia huku wanaongea. Jambo lililofanya Obama kuonekeana ni Rais wa aina yake.


2. OBAMA SINGING (Obama akiimba hadharani)

 

Kama ulikuwa haujui, Rais Obama ni mpenzi mkubwa wa muziki na mara kadhaa amelidhihirisha hilo mbele ya umati. Katika picha ya hapo juu, Obama aliimba wimbo wa "Jingle Bells" ikiwa ni usiku wa kusherehekea Sikukuu ya Noeli (Christmas).



Hata hivyo, alifanya hivyo tena wakati akiomboleza vifo vya Wamarekani weusi waliokuwa wameuawa bila kuwa na silaha yeyote. Alipokuwa akihotubia kanisani wakati wa misa ya kuaga miili ya victims hao, Obama aliimba "Amazing Grace" na kushangiliwa na wengi waliohudhuria misa ile.

3. SHADING A HURTFUL TEAR (Obama akilia baada ya watoto wadogo kuuwawa)



Wanasema kipimo cha uanamume sio nguvu tu, bali hata namna anavyoruhusu hisia zake kutawala, ndipo unapomjua ni mwanaume wa aina gani. Rais huyu hakusita kuonesha hisia zake baada ya kutokea massive shooting ambapo watoto wadogo zaidi ya 20, wenye umri wa miaka 6 hadi 7 waliuawa. Kutokana na kughubikwa na huzuni, Rais Obama alitoa machozi mbele za watu.

4. COMEDY ACTION COMMERCIAL FOR OBAMACARE (Obama akiigiza vichekesho ili kuwahamasisha vijana kwa bima ya afya)

 

Kwakweli nani kama Obama? Ukiachana na tabia yake ya kuwa katika uhalisia, Rais huyu ni mtu poa sanaaa. Katika kutaka vijana wengi kujiunga na ObamaCare ambayo ilikuwa ni project yake ya afya, Obama aliamua kuvaa uhusika wa vijana hao na kuact comedy iliyokuwa inalenga kushawishi vijana wengi. 



Katika video hiyo, Obama alionekana kufanya vitu mbalimbali kama watu wa kawaida, kama kujiangalia kwenye kioo akijaribu kuvaa na kuvua miwani, kujikonyeza na hata kujipiga selfie. Huyu ndo Obama bwanaaa!!!

5. #OBAMAANDKIDS (Obama na mapenzi yake kwa watoto) 

  


Yote tisa, kumi ni hili hapa! Rais Obama ni kati ya maRais ambao walikuwa wanapenda sana watoto na watoto walimpenda pia.

Kuna wakati aliitwa "The Whisperer," yaani mtu anaenyamazisha watoto kwani ilikuwa akibeba tu mtoto anaelia, basi kwishaaaa, mtoto huyu hunyamaza kabisa.

   

Obama mwenyewe amewahi kunukuliwa akisema kuwa, "Watoto wengi wanampenda kwasababu ana masikio makubwa kama vikatuni, hivyo wakimuona wanajua yeye ni kama katuni wanazozionaga kwenye TV." 


   

Mapenzi ya Obama kwa watoto na watoto kwa Obama sio ya nchi hii kwakweli. Hadi ulipofika muda wa yeye kuachia ngazi, kati ya vitu vilivyotrend mitandaoni ni pamoja na hashtag ya #ObamaAndKids.... daima atakumbukwa kwa upendo wake kwa watoto.

  



Tuambie, unakubali jambo gani zaidi kutoka kwa Rais Barrack Obama? Tupia comment yako sasa!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags