TUMEFIKIWA, tozo kwa vijana miaka 18 na kuendelea!

TUMEFIKIWA, tozo kwa vijana miaka 18 na kuendelea!

Eeeh bwana eeh! Tumefikiwa na sisi!!!

Kama mnavyojua, jana Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi.

Dk Mwigulu alisema hayo bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

Waziri huyo amesema ili kufikia azma hiyo wataanza kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania  kuanzia umri wa kuanzia miaka 18 kwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unaomtaka kila mwananchi mwenye umri huo wa au zaidi kujisajili.

“Napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi,”amesema

Waziri huyo amefafanua kuwa kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao.

Vijana mpo tayari???






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags