Tetemeko laua zaidi ya watu 40 Indonesia

Tetemeko laua zaidi ya watu 40 Indonesia

Tetemeko la ardhi limepiga kisiwa kikuu cha Java nchini Indonesia na kusababisha zaidi ya watu 40 kupoteza maisha na mamia kujeruhiwa, walisema maafisa wa eneo hilo.

Tetemeko hilo la kipimo cha 5.6 lilipiga mji wa Cianjur huko West Java, katika kina cha kilomita 10 (maili 6), kwa mujibu wa Data ya Utafiti wa Jiolojia ya nchini Marekani.

Tetemeko hilo lilisikika katika mji mkuu wa Jakarta, ambapo watu katika majengo ya miinuko mirefu walihamishwa. Maafisa wanaonya kuhusu uwezekano wa kutokea matetemeko mengine ya ardhi na idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags