Stumai Muki amtwanga chimwemwe Banda

Stumai Muki amtwanga chimwemwe Banda

Hehehehe! Nyie nyie  nani kasema wanawake hawawezi, basi bwana bondia mwanamke kutoka nchini Tanzania Stumai Muki ameshinda  katika pambano la ngumi, dhidi ya Chimwemwe Banda raia kutoka nchini Malawi kwa pointi katika pambano la raundi 8 la uzito wa kati ‘Super Fly’ lililofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Mara baada ya pambano hilo mwanadada Stumai amesema ametimiza kile alichokiahidi kwa Watanzania huku upande wa Chimwemwe ukidai kuwa kupoteza pambano haina maana mpinzani alikuwa bora zaidi bali imetokea tu.

Aidha, kupitia mpambano huohuo Mtanzania Grace Mwakamele nae amemshinda Luckia Ali kutoka  nchini Malawi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags