Snoop Dogg awashukuru Lamar na Drake

Snoop Dogg awashukuru Lamar na Drake

Mwanamuziki na producer wa #Marekani Snoop Dogg amewashukuru wasanii wenzake Kendrick Lamar na Drake kwa kurudisha muziki kwenye mstari.

Akiwa kwenye mahojiano yake na ‘Entertainment Tonight’, #Snoop ameeleza kuwa kufuatia na bifu la wawili hao limepelekea kurudisha tasnia ya muziki katika mstari wake huku akikazia kuwa nyimbo ambazo walikuwa wakizitoa za kurushiana madongo ziliimarishwa kuanzia uandishi hadi uandaaji.

Hata hivyo aliwashukuru Drake na Kendrick Lamar kwa kurudisha muziki wa Hip-hop katika chati na kuufanya usikilizwe zaidi duniani kote.

Ikumbukwe kuwa bifu la wawili hao lilianza baada ya #Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomsapoti #Drake kupitia album yake ya ‘For All The Dog’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags