Rais Nyusi afuta nyongeza ya mshahara wa 13 kwa wafanyakazi

Rais Nyusi afuta nyongeza ya mshahara wa 13 kwa wafanyakazi

Akihotubia Bunge, Rais wa Mozambique, Filipe Nyusi amesema anafuta nyongeza ya mshahara wa 13 kwa wafanyakazi, hatua hiyo imesababishwa na changamoto za kiuchumi na kusema watakaolipwa bonus hiyo ni wafanyakazi wasio na mikataba pekee.

Tangazo hilo linafuta rasmi utaratibu wa kila mwaka ambapo wafanyakazi wa Serikali wamekuwa wakilipwa marupurupu ya ziada kila mwishoni mwa mwaka.

Rais Nyusi aliliambia Bunge sababu ya kufuta mishahara hiyo kuwa nchi inakabiliwa na mzigo mkubwa wa mishahara na hivyo inajipanga kuweka uwiano sawa wa malipo kwa wafanyakazi bila kujali nyadhifa zao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post