Nape aeleza kuhusiana na mabadiliko ya bei za bando la internet

Nape aeleza kuhusiana na mabadiliko ya bei za bando la internet

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hakutakuwa na mabadiliko ya bei za bando yoyote hadi tathmini ya gharama itakapokamilika.

Tathmini hiyo inayofanywa kila baada ya miaka mitano, inatarajiwa kukamilika kati ya Desemba 2022 hadi Januari 2023.

Ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 21, 2022 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.

Nape amesema kwa sasa watoa huduma wote wako katika viwango vya bei elekezi iliyowekwa na Serikali ambayo ni kati ya Sh2.03 hadi Sh9.35.

“Hatutegemei mabadiliko yoyote kwa kipindi hiki hadi tathmini itakapokamilika, niwaombe wananchi wasione hatuhangaiki na suala hili, tumekuwa tukihangaika nalo.”

“Sasa tumefikia hatua ambayo tumesema tutatulia hadi tathmini itakapokamilika na matumaini yetu kuwa itatupa muelekeo mzuri,” amesema Nnauye.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post