MIMI MARS NA MARIOO WATHIBITISHA MAHUSIANO YAO

MIMI MARS NA MARIOO WATHIBITISHA MAHUSIANO YAO

Na Habiba Mohammed

Ebwana niaje watu wangu wa nguvu, another beautiful week na story motomoto. Kama kawaida maneno ya waswahili hayatokagi bure haswa pale waliposema mapenzi kikohozi.

Basi bhana moja ya story kubwa iliyokuwa ikizungumzwa katika mitandao ya kijamii ni kuhusu ukaribu wa mastaa wawili wa muziki wa bongo fleva, hapa mtoto bad maarufu Marioo na mtoto kutoka chuga Mimi Mars kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi baada ya wawili hao kuonekana pamoja katika maeneo mbalimbali ya bata.

Alooh! Basi jana kwenye tamasha la uzinduzi wa video ya mtoto bad, nae chuga queen hakuwa mbali alimsuprise kwa zawadi ya maua Marioo akiwa stejini na mabusu busu tele, mmmmh...

Licha ya wawili hao kukataa hawana uhusiano wowote wa kimapenzi kwa muda sasa, walimwengu wamebaki na maswali kupitia video inayowaonyesha wawili hao wakipeana mabusu hadharani na zawadi ya maua kwamba mastaa hao wameamua kuweka wazi uhusiano wao au ni moja ya maandalizi yaliyopangwa katika tamasha hilo?

Let me know kwa kudondosha comment yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags