Mbu wa malaria anawezekana kuwa chanzo cha ugonjwa wa mabusha

Mbu wa malaria anawezekana kuwa chanzo cha ugonjwa wa mabusha

Inasemekana kuwa chanzo kikubwa cha magonjwa ya mabusha ni vimelea vya minyoo jamii ya filaria, ambavyo vinaingia kwenye damu na vinaweza kusababisha maji kujikusanya sehemu za korodani.
 
Dhana ya kuwa maji ya madafu ni chanzo cha magonjwa hayo ya mabusha, lakini mganga mkuu mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume, anasema hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusiana na jambo hilo.
 
Anasema “Awali utafiti ulionesha mbu aina ya Culex ndio wanaosambaza minyoo husika, baadaye wataalamu wakabaini mbu wa aina zote wanaweza kusambaza vimelea hivyo, ndio maana tunasisitiza kuzuia mbu kwa kusafisha mazingira na kulala katika sehemu yenye chandarua.”
 
 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags