MAONI: Rayvanny hatopotea, bado ni WCB, Harmonize ajipange (Part 1)

MAONI: Rayvanny hatopotea, bado ni WCB, Harmonize ajipange (Part 1)

Na Leonard Musikula

Woza my people!!!leo siku njema sana na JICHO la tatu la Mwanachi Scoop lipo tayari kukuonesha kile kinachoweza kutokea mbele ili usije kushangaa baadae.

Ebhana eh, leo ngoja tuanze na hili la aliyekuwa msanii wa lebo ya Wasafi ambaye mwezi uliyopita kupitia mitando yake ya kijamii aliweka wazi kuachana na lebo hio na sio mwingine bali ni Rayvanny. Msanii huyu alikuwa chini ya lebo ya Wasafi Classsic Baby (WCB) tokea mwaka 2016 huku akiwa ni msanii wa pili kusainiwa na lebo hiyo ya mkali wa Bongo Flava - Diamond Platnumz. Usaili huo ni baada ya mwaka 2015 kusainiwa Harmonize, ambaye nae ameasi WCB mwaka jana.

 

Jina lake halisi anaitwa Raymond Shaban Mwakyusa ambaye alizaliwa tarehe 22 Agosti 1994, ambapo alianza kujulikana kupitia wimbo wake wa kwanza " Kwetu " ulitoka si siku nyingi sana tangu Harmonize atoe wimbo wake wa "Bado." Baadaye "Natafuta Kiki" huku safari yake kwenye muziki ilianza alipoingia chini ya usimamizi wa Tip Top Connection na baadae kuingia WCB Wasafi.

 

Rayvanny alishawahi kushinda tuzo ya BET 2017 katika kipengele cha International Viewer’s Choice na kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo hiyo kubwa.

Yes, unaweza kusema kuwa Vanny boy ndiye aliyapata mafanikio makubwa akiwa pale WCB kati ya wale waliondoka leboni hapo, ambao ni Harmonize na Rich Mavoko. Sasa kupitia mafanikio hayo yote aliyoyapata akiwa na WCB, Jicho la tatu la Mwananchi Scoop linaona kuwa huenda Vanny Boy ni WCB B au ni ‘Puppet wa WCB’ kiufupi bado yawezekana VANNY boy ni WCB kwa sababu zifuatazo:

 

  1. Kufungua Lebo akiwa bado yupo WCB

 

Rayvanny alifungua rasmi lebo yake ya muziki inayofahamika kama ‘Next level Music’ March 9 mwaka 2021, jambo lililowachanganya wafuasi wake ni kuwa huenda ilikuwa ni dalili za kusepa WCB lakini haikuwa hivyo kwa wakati huo.

Kama unakumbuka mwaka wa 2020, Meneja Mkuu wa WCB Diamond Platnumz aliulizwa kuhusu uwezekano wa Rayvanny kufungua lebo yake. Diamond alisema kuwa WCB itampa msanii yeyote msaada wa kufungua lebo yake. Kulingana na Diamond, WCB inawaruhusu wasanii ambao wako kwenye himaya yake kufanya hivyo.

Diamond alitoa mifano ya wasanii wa ng’ambo ambao wapo chini ya lebo kubwa na wapo na lebo zao binafsi, ikiwemo msanii Drake, ambaye yupo na lebo yake, Ovo Sound, lakini bado yuko chini ya lebo ya Young Money. P Diddy ana lebo yake ya Bad Boy Entertainment, lakini yuko chini ya Sony Music Entertainment.

Lebo ya NLM ilizinduliwa wakati Vannyboy anatamba na albamu yake, ‘Sound from Africa’, ambayo ina nyimbo 23. Wimbo wa mwisho kwenye albamu hiyo ni kollabo yake na Diamond Platinumz kwa jina “WOZA.”

 

“Kwahiyo WCB walimsaidia Vanny boy kufungua Lebo si ndio? Je WCB hawawezi kuwa na sharekwenye hiyo lebo yake na pia Lebo ya Vanny boy haiwezi kuwa WCB B? Haya maswali ukiweza kuyajibu basi tuyajue wote majibu yake.”

 

  1. Namna alivyoondoka na alivyoagwa na WCB

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny aliushukuru uongozi mzima wa Wasafi ukiongozwa na mkurugenzi mkuu , Diamond Platnumz na kusema kuwa;

“Miaka 6 sasa tangu tumeanza kufanya kazi pamoja na hii timu yangu, familia yangu, WCB Wasafi. Upendo, umoja vimekuwa nguzo kubwa saba kama timu. Mengi nimejifunza lakini pia mengi tumefanikisha tukiwa pamoja,” alisema msanii huyo kwa sauti isiyo ya kufurahisha, ya kuaga.

Rayvanny hakusita kuzungumzia baadhi ya mafanikio ambayo amepata akiwa kama mmoja wa familia kubwa ya WCB ambapo aligusia kwamba alifanikiwa kuwa msanii wa kwanza kushinda tuzo ya BET nchini Marekani na kuhimili kwa kutawala majukwaa mbali mbali ya kupakua na kusambaza miziki kama Boomplay.

 

“Shukrani za dhati kwa familia yangu Wasafi lakini pia kwa ndugu yangu Diamond Platnumz kwa kunipa nafasi dunia ione kipaji change nilichobarikiwa na mwenyezi Mungu ili kufika hapa nilipofika, kusaidia familia yangu na kufanikisha mengi katika maisha yangu,” Rayvanny alisikika akisema.

Kubwa zaidi ni kwa jinsi msanii huyo alimzungumzia bosi wake Diamond Platnumz ambapo alimshukuru pakubwa kwa kumuaminia miongoni mwa wasanii wengi na kumpa mkataba ndani ya pango la WCB ambapo ndilo chupa lililomtoa na kumfahamisha kwa mashabiki wengi alio nao sasa.

“Ndugu yangu Diamond Platnumz, heshima yangu kwako haitokaa ifutike, naudhamini sana mchango wako Mungu akusaidie, na yote uliyonifanyia, Mungu akuzidishie,” aliongeza kusema Rayvanny. 

Msanii huyo aliamua kutoka katika lebo ya Wasafi kwa njia moja ya kiheshima kimya bila kuzua mtafaruku kama ambavyo mwenzake Harmonize alifanya miaka mitatu iliyopita ambapo alizua tafrani na kukinukisha katika mitaa ya mitandaoni pakubwa huku akimdhihirisha Diamond kuwa mtu mbaya, jambo ambalo liliwakosanisha mpaka sasa.

“Ila naamini kwamba mtoto anayekuwa ni yule anayeondoka nyumbani kwenda kuanza maisha na kuiheshimu familia yake. Umenilea, umenikuza, sasa ni muda wangu wa kuondoka nyumbani na kuanza maisha mengine. Lengo ni ukuaji lakiji pia kuwapa nafasi vijana wengine, maana ninapotoka mimi, wengine wanapata nafasi ya kuingia lakini pia ninakokwenda, nitawashika mkono vijana wengine kwa sababu pia mimi nilisaidiwa kufika hapa,” alimaliza Rayvanny kwa sauti ya kuaga.

Jicho la tatu la Mwananchi Scoop lilijikita zaidi kutazama namna ambavyo wasanii na wana WCB watakavyorepond kuondoka kwake na chakushangaza WCB wote walionekana kuandika ujumbe wa kumpongeza kiheshima huku boss mkubwa Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika hivi; "Let us go president NLM" ikiwa na maana kuwa twenda pamoja Rais wa Next Level Music.

  

  1. Comments za mashabiki wa WCB

 

Mwaka 2019 Harmonize alipoamua kuondoka WCB, mashabiki wengi walionekana kuchukizwa na kitendo cha Harmonize kujiondoa Wcb Wasafi wakati wao ndio wamemuhangaikia kumkuza...Wengi wao wamesema akatafute mashabiki zake, mashabiki aliokuwanao sio wake bali aliwakuta Wcb na wakasema kuwa sio muda atapotea kwenye game ya music.

 

Lakini Kwa Vanny Boy imekuwa tofauti kabisa kwani mashabiki wengi wa WCB waliandika ujumbe wa kumtakia kila la heri Staa huyo wa mziki wa kizazi kipya, jambo ambalo linaonesha kuwa bado ataendelea kuwa na mashabiki wa WCB.

 

  1. Ukaribu wake na WCB

 

Kama ulikuwa unadhani kuwa baada ya kusepa WCB basi ndio anaweza kukata mahusiano ya Lebo yake ya zamani basi unajidanganya kwani ukifuatilia kwa kina utagundua kuwa bado ana mahusiano ya karibu na WCB kwani hata kwenye mitandao yake ya kijamii bado amewafollow wasanii wa WCB pamoja na viongozi wa WCB.

 

Vipi unaonaje mtu wangu? Je unadhani kuna mengi nyuma ya pazia? Endelea kufuatilia wiki ijayo kujua zaidi kuhusiana na siri hii kupitia jicho la tatu la Mwananchi Scoop.

 USIKOSE SEHEMU YA PILI.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post