Chini ya Serikali ya Rais William Ruto, waendesha mashtaka wameondoa kesi kadhaa dhidi ya baadhi ya washirika wake kwa misingi ya kesi hizo kukosa ushahidi.
Kuanzia Novemba 10, 2022, Mahakama ilikubali ombi la mwendesha mashtaka la kuondoa kesi ya ufisadi ya Ksh. Bilioni 7.4 dhidi ya Naibu Rais, Rigathi Gachagua, ikitaja ushahidi usiotosha.
Mnamo Mwezi Oktoba, DPP aliomba kuondoa mashtaka ya ufisadi dhidi ya Aisha Jumwa, ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, yanayohusiana na Ubadhilifu wa Ksh. Milioni 19.
Pia aliondoa kesi dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Samburu, Moses Lenolkulal, aliyeorodheshwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu.
Novemba 9, 2022, Aisha Jumwa alimtaka DPP kufutilia mbali kesi ya mauaji dhidi yake ambapo katika kesi hiyo, anashtakiwa pamoja na msaidizi wake kwa mauaji ya Bwana Ngumbao Jola wakati wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa wabunge 2019.
Leave a Reply