Inafahamika kuwa mwanamuziki Sebastian Charles 'Jaivah' ni miongoni mwa wasanii waliopita vizuri na upepo wa muziki wa Amapiano. Tangu ulipoanza kuvuma ukitokea Afrika Kusini.
Kupitia aina hiyo ya muziki Jaivah amefanikiwa kutengeneza ngoma ambazo zimekubalika mtaani mpaka duniani. Kutokana na utofauti wa sauti yake yenye uzito wa hali ya juu.
Uwezo wake kwenye muziki wa Amapiano ulitambulika kupitia wimbo wa Soup akiwa na Marioo, Chino, Scott London na Ks Hub. Ambao ulitoka Machi 4, 2023. Hata hivyo ameendelea kuaminika kwenye ramani ya muziki huo akifululiza kutoa ngoma kama vile, Pita kule, Buruda na kautaka.
Ngoma hizo zimefanya vizuri siyo tu Bongo bali hata nje ya mipaka hadi kufikia hatua ya ngoma yake 'Kautaka' kuwarusha wasanii wakubwa nchini Nigeria akiwemo Burna Boy, Mr Flavour, Tiwa Savage, Wizkid, Shallipo, Pocolee na wengine wengi.
Akizungumza na Mwananchi leo Februari, 25, 2025, Jaivah ambaye kwa sasa yupo nchini Nigeria amesema anafurahia ngoma yake 'Kautaka' kuendelea kuchana mawimbi ya muziki chini humo.
"Kautaka inaendelea kufanya vizuri, mimi nipo Nigeria sasa.Baadhi ya wasanii walio-vibe na ngoma yangu nimepata nafasi ya kukutana nao. Lakini na vitu vingine vinaendelea, pale itapopaswa kuwekwa wazi basi itakuwa wazi.
"Mwenyezi Mungu ajalie kama tutafanikiwa kufanya chochote basi kitaweza kutoka kwa sababu mimi kazi yangu ni kutoa burudani kwa watu," amesema Jaivah.
Jaivah kwa upande wake siyo kazi kubwa kutoa wimbo ambao unaweza kuvuma kwa haraka.
"Inaweza kuwa inawasumbua watu wengine. Lakini mimi natoa hit kama ngoma yangu ingine ninavyotoa, hata wakati naitoa niliitoa kama ngoma yangu kali ninayoikubali. Kwahiyo niliamini watu wataipenda. Kwa sababu hit ni uamuzi wa mashabiki,"amesema Jaivah
Ameongezea kuwa msanii anaweza kukaa studio akahisi wimbo anaotengeza ni hit lakini isiwe hivyo. Kwahiyo msanii hatakiwi kuwa na mataraijio makubwa sana anapotoa kazi," Jaivah
Baada ya nyimbo zake Buruda na Kautaka kufanya vizuri nchini Nigeria Jaivah amefanya ziara ya kimuziki nchini humo. Hii ikiwa mara ya pili sasa ambapo kwa mara ya kwanza alienda 2024, na kufanikiwa kupokelewa vizuri pia kutumbuiza majukwaa kadhaa.
" Nadhani wenzetu pia wanawaza sana ni wapi wanataka wafike yaani wanafanya muziki lakini pia wanawaza kufika mbali. Na mara nyingi huwezi kuwakuta nchini kwao utawakuta UK, Spain wakisambaza muziki wao na kutambulisha muziki wao sehemu nyingine," amesema Jaiva

Leave a Reply