Sababu Mj Kufunga Bandeji Vidoleni Wakati Wa Show

Sababu Mj Kufunga Bandeji Vidoleni Wakati Wa Show

Marehemu mfalme wa muziki wa Pop kutoka Marekani, Michael Jackson ‘MJ’ mara zote alipokuwa akipanda jukwaani alionekana wa kuvutia kuanzia mavazi, na hata miondoko yake wakati wa kutumbuiza.

Moja ya jambo ambalo limekuwa likionekana tofauti kutoka kwake ni kutumbuiza huku akiwa amefunga bandeji ‘mkanda mweupe’ mwishoni mwa vidole vyake. Hizi ndizo sababu za kufunga bandeji. Fahamu zaidi

Msanii huyo alifanya hivyo kama sehemu ya utambulisho wake. Kama ilivyokuwa kwenye soksi nyeupe katika kila show na kuvaa kofia wakati wote. Vidole vilivyofungwa mkanda/bandeji vilikuwa sehemu ya mwonekano wa kipekee jukwaani, na kuongeza upekee wa mtindo wake wa kisanii.

Mbali na hilo pia kwa mujibu wa Michael Bearden ambaye alikuwa Mkurugenzi katika ziara yake ya 'This Is It', alifunguka kuwa MJ alikuwa akifunga ncha za vidole vyake ili mashabiki waweze kufuatilia kwa makini dansi yake kuanzia mikononi hadi miguuni.

Aidha inaelezwa kuwa kutokana na umbali kutoka jukwaa lilipo na mashabiki, wasingeweza kuona harakati zote. Hivyo basi bandeji nyeupe zilikuwa kama utambulisho wake kama ilivyo kwa soksi nyeupe ambazo huzivaa kila show huku lengo kuu ni kuuvutia umma unaomuangalia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags