Kim Kardashian kulipwa zaidi ya million 466 kwaajili ya matumizi ya watoto

Kim Kardashian kulipwa zaidi ya million 466 kwaajili ya matumizi ya watoto

Mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian na Rapper Ye (Kanye West) wamefikia makubaliano ya pamoja ya talaka yao ambayo inahusisha malezi ya pamoja ya watoto wao na kugawana baadhi ya mali walizochuma pamoja.

Licha ya kwamba watawalea watoto wao watatu pamoja, Kanye atakuwa anampa Kim Kardashian pesa ya matunzo ya Watoto (Child Support) kila mwezi USD 200,000 ni sawa na Milioni 466. 8 za kitanzania kwasababu watoto hao watakuwa wanakaa muda mrefu na mama yao, New York Post imeripoti.

Aidha Reuters wameripoti kuwa watoto hawatoruhusiwa kutoka umbali wa zaidi ya KM100 kutoka nyumbani kwa Kim, Hidden Hills Los Angeles kabla hawajamaliza high school au kabla hawajafikisha umri wa miaka 19 lakini kila mzazi atakuwa anaweza kuwa pamoja na Wwtoto kwenye birthdays zao na matukio mengine ya muhimu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags