
Kendrick Lamar aweka rekodi mpya
Rapa wa Marekani, Kendrick Lamar ameweka rekodi nyingine kwenye muziki baada ya nyimbo zake zote kufikisha wasikilizaji bilioni 50 kwenye jukwaa la Spotify.
Rekodi hiyo inamfanya kuwa rapa wa tano kufikia mafanikio hayo, huku akiwa na nyimbo 11 zenye stream zaidi ya bilioni moja kwenye jukwaa hilo la Spotify.
Kwa mafanikio hayo ambayo yanatajwa kuwa ya kilegendari yanamfanya Kendrick kuungana na wasanii wengine wakubwa kwenye top 5 ya rapa wenye wasikilizaji wengi katika mtandao huo. Rapa wengine ni Drake akiwa na wasikilizaji 'Streams' bilioni 119, Travis Scott 59 bilioni, Eminem 58 bilioni, Kanye West 58 bilioni, na Kendrick Lamar 50 bilioni.
Mafanikio hayo yanakuja kutokana na kile ambacho wadau wengi wanasema ni bifu lake rapa Drake lililoanza mwanzoni mwaka 2024 na kufanikiwa kuuteka ulimwengu wa hip-hop.
Ambapo Kendrick aliachia wimbo ulioshinda tuzo tano za Grammy 2025 'Not Like Us', ulifuatiwa na albamu ya GNX iliyosifika sana. Pia alitumbuiza kwenye kipindi cha mapumziko cha Super Bowl, lakini ameendelea kufanya ziara ya albamu yake ya GNX ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa ziara zilizofanikiwa zaidi katika historia ya hip-hop.
Leave a Reply