Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji kwa ajili ya biashara

Weeeuuuuweeeeh! Kama kawaida yetu awamu hii tumekuja kivingine sio powa yaani, kwenye segment ya biashara tunakupatia fursa ambazo zitakukwamua kimaisha.

Watu wengi wanaamini kuwa mtaji ni lazima uwe na million au laki tano na zaidi, sasa leo nawajuza kuwa hata elfu hamsini au elfu 30 unaweza ukawa mtaji katika biashara yako na ukafika mbali, sasa leo tunakupatia fursa ya utengenezaji wa sabuni za maji za kufulia ili iweze kuwa biashara yako.

 

Mahitaji yanayohitajika
1. Salifoniki acid kilo 1
2. Sodash robo kilo
3. Maji lita 20
4. Slesi robo kilo
5.C.D.E vijiko vitano vya chakula

  1. Gricelini vijiko 15 vya chakula
    7. Chumvi ya viwandan kilo 1
    8. C.M.C vijiko vitano vya chakula
    9. Pafumu kijiko 1 cha chakula
    10. Rangi kijiko 1 chai

    Jinsi ya kuchanganya vifaa vyako
    1. Andaa ndoo ya plastik kisha weka salifonic acid,ikifuatiwa na sodash iliyochanganywa na maji na uanze kukoroga, weka maji na ukoroge mpaka vichanganyikane vizur

    2.wakati ukiendelea kukoroga weka sles,c.d.e na gricelin na uendelelee kukoroga

    3)Tia chumvi na uikoroge mpaka ilainike vizuri kisha weka c.m.c kidogo kidogo kwa kunyunyuzia huku ukiendelelea kukoroga,kisha weka rangi na perfumu na uendelelee kukoroga kwa dakika 10-15

    4)Baada ya hapo iache kwa saa 24 na itakuwa tayar kwa matumizi

    Kazi za malighafi hizo zinazotumika kutengenezea sabuni hiyo
    C.d.e kulaininisha maji
    Gricelin kulainisha nguo
    Chumvi kutia uzito
    C.m.c kuongeza uzito jinsi unavyotaka

Cha kuongezea kama tunavyo sema nunua vifaa vidogo kwa ajili ya majaribio ukishaona umeweza kabisa basi unaongeza kipimo kwa ajili ya biashara, tukutakie tu kila la kheri katika mapambano yako.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags