Mwanamitindo na mtangazaji wa Marekani, Amber Rose ameendelea kumuunga mkono Rais Donald Trump kwa kazi anayoifanya huku akidai kuwa wale waliokuwa wakimkosoa wakati wa uchaguzi sasa wametulia.
“Wakati wa uchaguzi, watu walinipiga vita sana, kwa kumuunga mkono Trump, sasa wale waliokuwa wananikosoa wametulia. Wanaona tayari ameanza kubadilisha nchi yetu kuwa bora zaidi,” amesema Rose
Rose mwenye umri wa miaka 41 anaamini jamii inapaswa kufungua macho na kuanza kuwa na mtazamo chanya kwenye kila kitu.
“Kwa bahati mbaya, watu ambao wanaunga mkono jambo zuri mara nyingi hukosolewa na kuonekana wako tofauti na wengine lakini kwa bahati nzuri kwangu sijali kabisa na nitasimama imara hadi mwisho bila kujali watu watanichukuliaje,” amemalizia Rose
Leave a Reply