Idadi ya watu nchini China yapungua

Idadi ya watu nchini China yapungua

Idadi ya watu nchini China imepungua kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, huku kiwango cha uzazi nchini humo kikifikia rekodi ya chini watoto 6.77 kwa kila wanawake 1,000.

Idadi ya watu mnamo mwaka 2022 ilikuwa bilioni 1.4118 na imepungua kwa 850,000 kutoka mwaka 2021.

Kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini humo kimekuwa kikipungua kwa miaka na hivyo kusababisha sera nyingi kupunguza muelekeo huo.

Lakini miaka saba baada ya kutupilia mbali sera ya mtoto mmoja, imeingia kile afisa mmoja alichoeleza kuwa zama za ongezeko hasi la idadi ya watu.

Kiwango cha watoto kuzaliwa mnamo mwaka 2022 pia kilipungua kutoka 7.52 mnamo 2021, kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya China, ambayo ilitoa takwimu hizo Jumanne.

Vifo pia vilizidi idadi ya waliozaliwa kwa mara ya kwanza mwaka jana China iliingia katika kiwango cha juu zaidi cha vifo tangu mwaka 1976 vifo 7.37 kwa kila watu 1,000, kutoka 7.18 mwaka uliopita.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags