Haya ndo mavazi ya wanaume yanayowavutia wanawake

Haya ndo mavazi ya wanaume yanayowavutia wanawake

Ni siku nyingine tena tunakutana kupitia safu hii, nikiamini kuwa u mzima wa afya tele na unaendelea na majukumu yako ya kulijenga taifa.

Tumekuwa tukijuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya mitindo, urembo na mavazi ambayo najua huenda unayajua ila mimi nakujuza tu zaidi.

Leo tutaangalia aina mbalimbali ya mitupio kwa wanaume ambayo upendwa zaidi na wanawake endapo ikivaliwa kwa ufasaha na kufuata taratibu zote.

Wataalamu wa mambo ya mitindo wanawaelezea wanawake kama ni watu wanaopenda sana kuvaa na kupendeza japokuwa sio wote ila kwa asilimia kubwa wanajitahidi kwenye kutupia kama ilivyo kwa wanaume.

Tukumbuke kuwa kuvaa sio jambo gumu ila shida inakuja pale ni nguo za aina gani mtu anapaswa kuzivaa kulingana na mazingira na jinsi alivyo ili kuweza kuleta muonekano mzuri na wakuvutia  katika jamii inayotuzunguka.

Hivyo wewe mwanaume usije ukashangaa siku ukivaa moja wapo ya mavazi haya nitakayoyasema ukawa unaangaliwa sana na watu wenye jinsia ya kike. 

Moja ya mavazi ambayo wanawake wengi wanapendelea wanaume wavae ni jinzi na t- shirt, kama mwanaume akipangilia vazi hili vizuri basi muonekana wake utakuwa wa kuvutia na nadhifu muda wote na utawavutia wanawake wengi.

Aina nyingine ya mavazi ni pale mwanaume anavaa jinzi kali akiwa na shati ambalo juu yake anaweka koti la suti huku chini akiwa amevaa raba au viatu vigine vizuri, hakika mavazi hayo pia uwavutia wanawake.

Pia lipo vazi la suti, hapa kama mwanaume akishona au kununua vazi  na kisha kuchagua rangi inayopamba na kuendana na ngozi yake pamoja na kupangilia  ataonekana nadhifu na wa kuvutia.

Najua unafahamu kuwa vazi hili la suti uvaliwa katika shughuli mbalimbali ambazo ni maalumu basi nakushauri wewe mwanaume pendelea kulivaa katika shughuli hizo kwani linawavutia sana wanawake.

Aina nyingine ni pale wanaume anaposhona shati la kitenge na kuvalia na suruali inayoendana na rangi ya kitenge hicho, hakika vazi hili linapopangiliwa vizuri uonekana la kuvutia.

Vilevile lipo vazi la kaptula na t-shirt, vazi hilo nalo ni zuri na wanawake wengi upenda wanaume walivae hasa katika siku za mapumziko au pindi wanapokwenda ufukweni.

Ikumbuke kuwa katika mavazi yote haya ili onekana nadhifu ni muhimu yakawa safi na yaliyopangiliwa vizuri.

Natambua lipo tatizo la wanaume wengi kushindwa kwenda na wakati kwa kuvaa mavazi yanayovutia hivyo kupitia safu hii ya leo najua watakuwa wamejifunza kitu. Tukutane tena siku nyingine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags