Aliyemvamia Burna Boy Stejini Afunguka

Aliyemvamia Burna Boy Stejini Afunguka


Shabiki aliyemvamia mkali wa Afrobeat Nigeria Burna Boy stejini na kupelekea msanii huyo kususia show na kushuka jukwaani amefunguka kuwa alipanda katika steji hiyo kwa lengo kuonesha mapenzi kwa msanii huyo.

Kufuatia na video inayoendelea kusambaa mitandaoni imemonesha shabiki huyo akieleza tukio zima huku akidai kuwa hakuwa na nia ya kumuumiza Burna bali alipanda stejini kwa lengo la kuonesha upendo kwa msanii huyo.

Lakini pia aliweka wazi kuwa alipanda stejini hapo kumuomba Burna atumbuize naye kwani na yeye ni msanii chipukizi ambaye anatamani kufikia mafanikio ya Burna.

Utakumbuka kuwa Burna alisusia Show iliyofanyika Desemba 31, 2024 baada ya shabiki huyo kumvamia jambo ambalo liliwaacha njia panda mashabiki, lakini kupitia ukurasa wa Instagram wa Burna alitoa maelezo kuhusu tukio hilo akida kuwa muda wake wa kutumbuiza ulikuwa umekwisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags