Whatsapp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi!

Whatsapp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi!

Mtandao unaokubalika zaidi duniani kote wa WhatsApp umetangaza kuacha kufanya kazi katika simu za zamani za Android ambazo hazipati Updates za mfumo mpya unaofanyika kila mwaka.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuanzia Januari 1, 2025, itaacha kutoa huduma katika simu za aina hiyo lengo likiwa ni kuleta vipengele na huduma mpya zinazohitaji vifaa vya kisasa na kuachana kabisa na mifumo ya zamani.

Simu ambazo zitakazofungiwa ni pamoja na (Samsung: Galaxy S3, Galaxy Note 2, Galaxy Ace 3, Galaxy S4 Mini), (Sony: Xperia Z, Xperia SP, Xperia T, Xperia V), (LG: Optimus G, Nexus 4, G2 Mini, L90), (Motorola: Moto G (1st Gen), Razr HD, Moto E 2014) na (HTC: One X, One X+, Desire 500, Desire 601).

Mbali na mtandao huo kuacha kufanya kazi katika Android lakini pia kwa watumiaji wa simu za Apple (Iphone) zenye mfumo wa iOS 15.1 mwisho wa kutumia mtandao huo ni mwezi Mei 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags