Dr. Dre kutunukiwa nyota ya heshima, hollywood walk of fame

Dr. Dre kutunukiwa nyota ya heshima, hollywood walk of fame

Producer na ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Dr. Dre anatarajiwa kutunukiwa nyota ya heshima kwenye Hollywood Walk of Fame Machi 19, mwaka huu katika Jengo la Hollywood Boulevard.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa Dr. Dre atatunukiwa nyota hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya muziki.

Mshindi huyo wa Grammy mara tisa pia atatunukiwa nyota hiyo ya 2,775 kutokana na kuwainua wasanii wenzake kupitia rekodi lebo yake ya ‘Aftermath Entertainment’ ya mwaka 1996, ambayo ilifanikisha kuwaleta mjini mastaa mbalimbali akiwemo Eminem, 50 Cent, Kendrick Lamar, na Anderson, Paak na Jimmy Iovine.

Dr. Dre ataungana na mastaa Macaulay Culkin, Ludacris, Martin Lawrence, Michael B. Jordan, 50 Cent, marehemu Tupac, Snoop Dogg, Kevin Hart, Pharrell Williams na wengineo ambao wametunukiwa tuzo hizo.

Hollywood Walk of Fame ni eneo la kutembea kwa miguu kando ya jengo la Hollywood ambapo zinawekwa nyota za mastaa waliofanya vizuri katika upande wa burudani, kama vile waigizaji , waandaji filamu, wanamuziki, watayarishaji wa muziki nk.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags