Zuchu Na Ujumbe Huu Kwa Mashabiki Wanaomkosoa

Zuchu Na Ujumbe Huu Kwa Mashabiki Wanaomkosoa

Baada ya mwanamuziki Zuchu kuachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Amanda’ ambayo haijapokelewa vizuri na baadhi ya mashabiki wakiunanga kuwa wimbo huo ni mbaya, hayimaye msanii huyo ametoa tamko akiwataka mashabiki wanaomkosoa kuacha kufuatilia nyimbo zake.

Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram muda mchache uliyopita amechia ujumbe akieleza kuwa ameamua kuwa tofauti hivyo mashabiki zake wanatakiwa kupokea mabadiliko hayo.

“Nitoe tu Tamko kwa mashabiki zangu, huyu ndio mimi mpya, nitakuwa nabadilika kadri nitakavyotaka na kama unahisi mabadiliko haya huyawezi mimi kama msanii nakushauri tu ni bora uniache sasa .Maana huko mbele nnavoenda kuviachia ndo hutovielewa kabisa.

“Mnadumaza hii industry kwa mazoea dunia inatuacha na tunapenda mno kujifanya wajauaji nimechoka kuimba vitu vile vile kila siku Na kukaa kwenye confort zone sitaki tena i will challenge my sound kila siku,”ameandika

Aidha ameongezea kwa kueleza “Na kwa nyie wa hizi ndo zitaleta Grammy tafadhali feel free kushabikia Msanii unaeona anavigezo vyako vya Grammy uzuri East Africa tumebarikiwa wasanii wengi wakali so .Kwa yeyote Unaenisapoti i love you funga mkanda maana safari ndo kwanza imeanza #Malengo,ameandika Zuchu

Wimbo huo ambao umeachiwa saa 23 zilizopita ukiwa na zaidi ya watazamaji 208,900 katika mtandao wa YouTube umepokea maoni tofauti katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wakieleza kuwa wimbo huo ni mbaya.



“Hii nyimbo unaweza itumia kama alarm kabisa hasa kwa tunaoishi kimara,” mwingine akiandika “Nahisi umesahau kazi yako kuna muda nahisi unaimba tu kujifuraish mwenyew sasa iki nini jamani. Kiukweli huu wimbo ni mbaya, “Tuweke ushabiki wa kijinga nyimbo mbayaaaa uchizi si uchizi utahila si utahila πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ Yani kwa vile unajina basi unaona kila utakachoimba Sawa tuuu tutakupokea tumeshazindika sasa,”

Huku wachache wakiusifia kwa kuandika “Hii nyimbo nimeipenda sanaπŸ‘ŒπŸ½, since morning nimeamka like… Aaagghhh naliaaaaa eeeehhh naumia πŸ˜‚πŸ˜‚. Hivi sasa tuko tunasaidiana na Mozzah kuanguka Aaaghhh naliaaaaa πŸ˜…πŸ˜…πŸ’ƒπŸ½πŸ•ΊπŸ’ƒπŸ½,” , “Anaanzaga hivi hivi na tutasema ni mbaya ila baadae inakuja kuwa hit songπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ AMANDAAAAAA,”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags