Utafiti: Asilimia 50 Ya Wanawake Wanamichepuko

Utafiti: Asilimia 50 Ya Wanawake Wanamichepuko

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na jukwaa la mahusiano la OnePull, umebaini kuwa asilimia 50 ya wanawake ambao wapo kwenye ndoa au mahusiano wanadaiwa kuwa na wapenzi wa akiba ‘Michepuko’.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanawake wengi wanaeleza kuwa michepuko hiyo ni watu ambao wamewahi kutoka nao kimapenzi ‘EX’ au mtu yoyote wanayemuamini ambaye anaweza kumpa faraja endapo uhusiano wake ukivunjika.

Utafiti huo uliohusisha zaidi ya wanawake 3,000 kutoka mataifa mbalimbali, ulibaini kuwa sababu kuu zinazowasukuma wanawake kuwa na wapenzi wa akiba ‘Michepuko’ ni pamoja na hofu ya kuachwa bila taarifa, mahusiano yasioeleweka na kutokuwa na hisia na wapenzi wao.

"Hili si suala la usaliti moja kwa moja kwa kila mtu, bali mara nyingine huwa ni hisia ya kutaka usalama wa kihisia na kuwa na mtu wa kuzungumza naye kwa karibu," ilisema ripoti hiyo.

Hata hivyo, wataalamu wa mahusiano wameonya kuwa tabia hii inaweza kuharibu uaminifu katika uhusiano, na kusababisha migogoro ya kimapenzi au kuvunjika kwa ndoa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags