Zuchu Atuma Barua Ya Wazi Kwa Diamond

Zuchu Atuma Barua Ya Wazi Kwa Diamond

Mwanamuziki Zuchu ametuma barua ya wazi kwa bosi wake na msanii Diamond kufuatia na yanayoendelea katika mitandao ya kijamii kuhudiana na maswala mazima ya yeye kutaka kuolewa na msanii huyo.


Kuputia ukurasa wake wa instagram Zuchu ameweka wazi kuwa kitendo hicho kinachoendelea kupewa kipaumbele kwenye kipindi cha Mashamsham kinamuumiza kiafya ya mwili na akili.

“@diamondplatnumz KWAKO KIONGOZI. Kinachoendelea sasa Mitandaoni kupitia maudhui ya kipindi chenu Mashamsham kimekua kama sehemu ya kuniumiza na kunididimiza kisanaa na kiafya ya Mwili Na akili.


Lakini nasema nashukuru na nimeyapokea yote. Nimekua msanii wa taasisi mwenye kasi na mwenye kuipambania kazi yangu licha ya uwekezaji unaofanywa na kampuni yenu sikatai ni jambo kubwa na la kheri kumkomboa binti mwenye kipaji kwa kumuwekezea lakini nauliza Je, ni haki hiko kutumika kama silaha pia. Au niliwakosea nini mpaka kufikia kunifanyia Bullying na harassment hizi. Nasibu familia yako wanabaya langu lipi ambalo wanaona ni haki wao hata wakiwa na mahojiano binafsi kutokueka stara ya mambo yangu, na huwa wanahakikisha hawakuharibii wewe bali mimi,” ameandika Zuchu

Aidha hakuishia hapo alifunguka kuhusiana na tasisi hiyo kuendelea kumchafua mara kwa mara licha ya kufikisha taarufa kwa kiongozi huyo lakini hakuna lililofanyika.

“Nimefikia hatua leo naandika barua ya kisheria Kwa walezi wangu sababu ya ukandamizaji wa mara kwa mara juu yangu Inauma sana, nitaenda mahakamani na pengine sitaweza kushinda taasisi yenu yenye nguvu lakini hata nikishindwa huko Namuachia MWENYEZI MUNGU yeye ndo Hakimu wa mwisho.

ASANTENI NASHUKURU kwa kuendelea kunibully na kuniharrass. Nishaomba Sana kwako kama kiongozi lakini mara nyingi maombi yangu hugonga mwamba na kunatengenezwa Content za kusudio la kunivunjia heshima, Kuniumiza na kuharibu afya yangu ya akili. Mimi ni binti na mwanamziki pia, sijawahi kuona media yoyote inaniharras kama ambavyo media ya taasisi yenu mmekua mkifanya.
Sina cha kuwafanya kikubwa nyinyi ni wenye Nguvu Na mimi Namshitakia Mwenye Ukuu, utukufu zaidi yangu na ninaenuamini zaidi M/MUNGU .ASANTENI SANA NASHUKURU,” amemalizia Zuchu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags