Aliyekuwa mhudumu wa shirika la ndege la ‘Alaska Airlines’ Nelle Diala amefukuzwa kazi baada ya video yake akiwa anakatika viuno (kucheza) kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Video hiyo ambayo mhudumu huyo aliishare kwenye mtandao wa Tiktok imemuonesha akiwa anacheza wimbo wa ‘Ghetto’ ulioimbwa na E.K.E jambo ambalo lilipelekea waajiri wake kumfuta kazi kwa kukiuka sera za katika kampuni hiyo.
“Nilieleza kuwa video hiyo haikukusudiwa kudhuru mtu yeyote au kampuni, lakini hawakutaka kusikiliza. Mwajiri wangu alinishutumu kwa kukiuka sera yao ya mitandao ya kijamii.
Kupoteza kazi yangu kuliniumiza sana. Siku zote nimekuwa mwangalifu kuhusu kile ninachoshiriki mtandaoni, na sikuwahi kufikiria kuwa video hii, ambayo hata haikutaja shirika la ndege kwa jina, ingegharimu kazi yangu. Sasa, ninajaribu kufikiria jinsi ya kusonga mbele,” alisema Diala
Kwa sasa mwanadada huyo amefungua tovuti aliyoipa jina la 'GoFundMe' ili watu wamchangue pesa kipindi hiki ambacho hana kipato akitafuta kazi kwenye kampuni nyingine ambapo mpaka kufikia sasa anadaiwa kuingiza zaidi ya dola 2,000.
Leave a Reply