Filmu iliyochezwa na marehemu mkali wa Hip Hop Marekani Tupac Shakur iitwayo ‘JUICE’ imetimiza miaka 33 ambapo ilitoka rasmi siku kama ya leo Januari 17 mwaka 1992.
Filamu hiyo ambayo ilikuwa ya kwanza kwa mkali huyo ilionesha kipaji chingine cha Pac katika uigizaji akicheza nafasi ya muhusiaka mkuu aitwaye Roland "Bishop".
Hivi ndivyo Pac alivyoelezea uhusika wake:
"Mhusika wangu ni Roland Bishop, mtu wa kisaikolojia, asiye na usalama, mwenye vurugu nyingi, na hasira ya haraka. Bishop alitaka tu kupata heshima. Alitaka heshima ambayo baba yake hakupata. Kila kitu alichofanya, alifanya ili kujipatia sifa.
Nilishangazwa mwenyewe kwa kupata nafasi hiyo. Sikuiamini. Hadi sasa siamini. Bado natembea mitaani, na mtu akiniona, nahisi kutokuwa na raha. Kisha nakumbuka, 'Oh, filamu.' Sitaigiza nafasi kama hiyo tena, isipokuwa kutakuwa na mwendelezo."
"Juice" ilikusanya zaidi ya dola milioni 8 mwishoni mwa wiki ya ufunguzi na ilipata zaidi ya dola milioni 20 kwenye box office. Filamu hiyo iliyoongozwa na Ernest Dickerson iliwakutanisha mastaa mbalimbali akiwemo Samuel L. Jackson, Queen Latifah, Grace Garland, Ernest Dickerson, Khalil Kain na wengineo.
Mkali huyo hakuishia hapo kwenye uigizaji alionekana tena kwenye filamu kama Poetic Justice, Above the Rim, Bullet, Gridlock'd na nyinginezo.
Ikumbukwe kuwa Tupac alizaliwa Juni 16, 1971 na alifariki September 13, 1996 akiwa na miaka 25, huku kesi ya mauaji ya kifo chake bado inaendelea mahakaman
Leave a Reply