Diamond Anaingiza Mkwanja Huu Youtube

Diamond Anaingiza Mkwanja Huu Youtube

Mwanamuziki anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi Diamond ameripotiwa kuingiza mkwanja mrefu kupitia mtandao wa kusikiliza na kutazama muziki wa YouTube.

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Africa Fact Zone’ Diamond ameshika nafasi ya tatu kama staa nayepokea mkwanja mrefu ambapo ametajwa kuingiza dola 2.7 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 6.8 bilioni kwa mwaka mzima.

Orodha hiyo ambayo imeongoza na binti mdogo anayeipperusha bendera ya Afrika Kusini, Tyla ambaye anaingiza dola 3.1 milioni huku namba mbili ikishikwa na Mohamed Ramadani kutoka Misri ambaye anaingiza dola 2.8 milion.

Mbali na hao wapo mastaa wengine ambao ni pamoja na Burna Boy (dola 1.5 milioni), Rema (dola 924,700), Davido (dola 902,100), Fally Ipupa (dola 1 milioni), Sherine (dola 1 milioni), Kizz Daniel (dola 1.2 milioni) na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags