Mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes ameripotiwa kujisalimisha kwa polisi, baada ya kumpiga mfanyakazi wake aitwaye Dashiel Gables tukio lililotokea Ijumaa, Januari 10, katika ukumbi wa jengo la Gables Dumbo, Brooklyn jijini New York.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ mapema wiki hii Busta alijisalimisha kwa Polisi wa New York (NYPD) na kupewa hati ya mashtaka ya shambulio la daraja la chini pamoja na unyanyasaji huku akiruhusiwa kwenda nyumbani mpaka pale atakapopewa tarehe ya kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza mashitaka hayo.
Busta alimchapa Gables baada ya mfanyakazi huyo kutumia simu (kuchati) wakati wa saa za kazi jambo lililopelea kuleta mzozo na baada ya muda raha huyo alimpiga Gables na kumuumiza jicho la kushoto.
Hata hivyo baada ya kumpiga mtu huyo Busta alidaiwa kukimbia eneo la tukio ndipo Gables aliamua kuita polisi na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu, aidha polisi wameweka wazi kuwa wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Leave a Reply