Hatimaye mwigizaji Aaron Pierre amefunguka kuhusu video yake ya 'That Mufasa' inayosambaa kwenye mtandao ya kijamii na vutia wengi. Video ambayo ilipatikana kwenye kipindi cha JHud Show cha kwake Jennifer Hudson.
Pierre kupitia mahojiano ambayo amefanya na 'Extra' wakati wa tuzo za heshima za filamu kwa watu weusi nchini Marekani, amesema anawashukuru mashabiki kwa kuifanya video yake kuwa maarufu mtandaoni.
"Nahisi upendo na furaha wakati wowote watu wanaponisalimia hivyo, wakati wowote watu wanashiriki nami. Ilikuwa wakati mzuri nashukuru na nifuraha kwamba iliwagusa watu wengi walifurahia wakati huo ni jambo zuri," amesema Pierre.
Hata hivyo, ameongezea kuwa kipindi cha "Jennifer Hudson Show" kililazimika kufunga sehemu ya maoni kwa mara ya kwanza kwenye video yake iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana kuwepo na maoni mengi kuliko kawaida.
“Ndiyo mara ya kwanza kusikia hivyo na sijui niseme nini naamini kabisa ni furaha sana nimepokea na ninashukuru kwa hilo. Unajua, ni jambo maalum. Kwa hiyo, asante,”amesema Pierre
Video hiyo ya Pierre katika 'JHud Show' imekusanya mamilioni ya watu kuipenda kwenye TikTok ikipokea maoni zaidi ya milioni 37.

Leave a Reply