Diamond Hataki Unyonge

Diamond Hataki Unyonge

Wakati maandalizi ya utolewaji tuzo za Trace yakiendelea kisiwani Zanzibar. Moja ya tukio ambalo limepokea maoni mengi kutoka kwa mashabiki na mastaa ni kuhusiana na mwanamuziki Diamond kusafirisha gari (ndinga) zake kutoka Dar hadi Zanzibar.

Kupitia komenti mbalimbali katika mitandao ya kijamii mashabiki wamempongeza msanii huyo kwa kutokuwa mnyonge huku wakiandika.

“ Hakuna mnyonge wamekuja nchini kwetu lazima wanyooke”, “Ili libaba limeona lipeleke utajiri wake huko”, “Nadhani Watanzania washajua ukubwa wa Diamond kwa sasa kila mtu anamuongelea yeye na tuzo zenyewe wasanii wageni wanamtaja yeye tu,”



Mbali na mashabiki kutoa komenti zao naye mwanamuziki Harmonize alifurahishwa na kitendo hicho cha Simba kusafirisha ndinga zake huku akijiululiza kama zimepaa au zimeogelea.

“Najivunia sana wewe broskizo, nadhani nimesoma zaidi kuhusu show, nawaza zimepaa au zimeogelea. Wewe ni makini sana na kweli nataka kukutana na wewe leo,” ameandika Konde Boy

Mkali huyo ambaye anashindanishwa kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka kupitia ngoma ya ‘Komasava’ amesafirisha ndinga zake tatu ambazo ni Simba, Simba 1 na Simba 2 ambayo haiingi risasi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags