Rapa kutoka Marekani, Tory Lanez amehamishwa gereza jingine baada ya maafisa kuhofia usalama wake katika gereza la California Correctional Institution.
Kwa mujibu wa TMZ, rapa huyo amehamishwa gereza kutoka la awali hadi California Men’s Colony (CMC) kwa ajili ya usalama wake. Ingawa bado hajapona lakini wakili wake ameeleza kuwa kwasasa anaendelea vizuri kidogo.
Ikumbukwe Mei 12, 2025 Tory alijereuhiwa kwa kuchomwa kisu mara 14 na mfungwa mwenzake aliyejulikana kama Santino Casio, ambapo alipata majeraha mgongoni, kifuani, kichwani na usoni na kwenye mapafu.
Tory Lanez anatumikia kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake na rapa Megan Thee Stallion mwaka 2020.

Leave a Reply