Mwanamuziki wa nyimbo za Taarabu na mwigizaji nchini Hanifa Maulid ‘Jike la Chui’ ameweka wazi sababu ya muziki huo kushuka akitaja kuwa ni wasanii wenyewe kushindwa kuupa promo.
Akizungumza na Mwananchi Jike la Chui ameeleza kuwa wasanii wa Bongo Fleva wamekuwa wakiupushi muziki wao mitandaoni lakini hiyo ni tofauti kwa wasanii wa muziki wa taarabu.
“Sababu ya muziki wa taarabu kushuka ni sisi wenyewe hatuendi kidigitali, wenzetu wanamuziki wa Bongo Fleva wanapromote nyimbo zao kwa kuziweka kwenye mitandao kama Audio Mark, wanazifanyia challenge lakini kwa upande wetu hatufanyi hivyo ukizingatia soko limebadilika,”amesema
Aidha ameongezea akieleza kuhusina na tetesi katika mitandao ya kijamii zinazodai kuwa muziki huo unadidimizwa na mabifu baina ya wasanii na vikundi vya taarabu.
“Kuhusu mabifu kuporomosha taarabu inawezekana kuwa kweli lakini mbona wenzetu wa Bongo Fleva wanayo mabifu yao lakini kazi zao zinaenda na wanafanya muziki wao usiyumbe, mimi nadhani muziki wetu unapendwa ni sisi tuu wenyewe kubadilika na kurekebisha madhaifu yetu,”
Akizungumzia kuhusiana na uhusika wake katika tamthilia ya ‘Kombolela’ mwanamuziki huyo ameeleza kuwa filamu hiyo imempa mafanikio makubwa na kuinua maisha yake kwa ujumla.
“Ni filamu yangu ya kwanza na kipaji hichi cha uigizaji kilitambuliwa na familia yangu. Kusema ukweli Kombolela ni kama mkombozi wangu nimepata mafanikio makubwa vilevile kupitia filamu hiyo, kwanza imepanua wigo wa Sanaa yangu, rizki zimekuwa nyingi nachukuliwa sehemu tofauti tofauti kikazi nje ya uigizaji na hii yote ni kutokana na ‘Kombolela’,” amesema
Ushauri kwa wasanii wanaotaka kuingia kwenye taarabu na uigizaji
“Wanaotaka kuingia kwenye taarabu, niwanakaribisha, chamsingi kama umeamua kuimba taarabu basi inabidi ufanye juhudi nauwe na nia uvumilivu, subra uwe na moyo mkomavu, Sanaa inahitaji heshima.
"Kwa upande wa uigizaji vilevile heshima na ukiingia ufate kilichokupeleka sio unaingia ili upate jina la kuuzia biashara, haukatazwi kufanya biashara ila usiingie kwaajili ya kuuza sura ukiingia fanya kazi kweli kweli ili kuiinua sanaa ya uigizaji,”amesema
Aidha ameongezea kwa kueleza “Miaka mitano mbele sanaa ya uigizaji naiona mbali sana sidhani kama Watanzania wataangalia tamthilia au movie za nje sidhani. Na ndio maana mtu akipata nafasi ya kuigiza anafanya kweli na msanii yoyote akipata nafasi usiiachie igiza kama hautoigiza tena,”
Jike La Chui ametambulika kupitia nyimbo zake mbalimbali ikiwemo Ishu Pambe, Stop Red Kadi, Makavu Live, Naufunga Mtaa na nyinginezo. Huku akiigiza kwenye ‘Kombolela’ kama Chiku mtoto wa mzee Kikala

Leave a Reply