Kid Cudi, ambaye jina lake halisi ni Scott Mescudi, alieleza kuwa gari yake aina ya Porsche iliwashwa moto baada ya bomu aina ya Molotov kurushwa ndani.
“Paa la juu la Porsche yangu lilikatwa na ndipo walipoingiza bomu la Molotov, baada ya hili Niliwasiliana na Sean Combs nikamwambia kuwa tunahitaji kukutana tuzungumze na tulimalize hili maana hali ilishakuwa ya hatari,”amesema Cudi.
Mbali na tukio hilo Cudi aliweka wazi kuwa Diddy alivamia nyumba yake kwa hasira na wivu baada ya kugundua rapa huyo ana uhusiano na mpenzi wake wa zamani Cassie Ventura ambapo alivamia nyumba hiyo na kuharibu kamera za usalama na kumfungia mbwa wake bafuni.
Baada ya tukio hilo Cudi alikutana na Diddy ‘Soho House’ kwa ajili ya kuzungumza lakini Combs alikana kufanya tukio hilo lakini alionyesha tabia ya kutisha, ambayo Cudi aliifananisha na ‘Marvel supervillain’ (adui wa Marvel”.

Combs, mwenye umri wa miaka 55, atakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani endapo atapatikana na hatia katika mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, uhalifu wa kupanga na mashtaka mengine. Lakini rapa huyo amekana mashtaka yote dhidi yake.
Utakumbuka Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn.
Leave a Reply