Soksi Ya Michael Jackson Yauzwa Sh21 Milioni

Soksi Ya Michael Jackson Yauzwa Sh21 Milioni

Soksi moja ya mfalme wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson ambayo aliivaa wakati wa tamasha nchini Ufaransa miaka ya 1990 imeuzwa kwa zaidi ya dola 8,000 sawa na Sh21 milioni.

Dalali wa soksi hiyo tokea Ufaransa amesema MJ alivaa soksi hiyo yenye rangi ya krimu iliyopambwa kwa vito vya kung’aa wakati wa tamasha la muziki la 'HIStory World Tour' lililofanyika mwaka1997.

Inaelezwa kuwa soksi hiyo iliokotwa na fundi mmoja ikiwa imetupwa karibu na chumba alichobadilishia nguo Michael baada ya tamasha hilo kutamatika katika mji wa Nimes dalali Aurore Illy aliiambia AFP.

Hata hivyo MJ alionekana akiwa amevalia soksi hiyo kwenye baadhi ya vipande vya video wakati akitumbuiza kwenye tamasha hilo wimbo wake wa "Billie Jean".

Miaka kadhaa baadaye, soksi hiyo imeuzwa tena kwa pesa ndefu huku dalali Aurore Illy akisema soksi hiyo inaweza kutumika kama ibada kwa mashabiki wa Michael Jackson.

"Kwa kweli ni kitu cha kipekee soksi hiyo inaweza kuwa hata ibada kwa mashabiki wa Michael Jackson," alisema Illy.

Soksi hiyo, ambayo awali ilikuwa na thamani ya dola 3,400-4,500 iliuzwa kwa dola 8,822 katika moja ya nyumba za mnada mjini Nimes Jumatano, Julai 30, 2025.

Utakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa vitu vya Michael Jackson kupigwa mnada mwaka 2009 kituo cha michezo cha Macau kililipia dola 350,000 ili kununua glavu ya kumeta meta ambayo MJ alivaa wakati akitumbuiza ngoma yake ya kwanza ya 'moonwalk' mwaka 1983. Pia kofia aliyovaa kabla ya maonyesho hayo iliuzwa kwa zaidi ya dola 80,000 huko Paris mwaka 2023.



Michael Jackson alifariki dunia mwaka 2009 akiwa na miaka 50. licha ya kifo chake na tuhuma za unyanyasaji wa watoto wakati wa uhai wake, bado mfalme huyo wa Pop duniani anawafuasi wengi ambao mpaka leo wanaendelea kuonesha mapenzi yao kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags