Mtangazaji na mfanyabiashara Marekani Paris Hilton amerudi kwenye nyumba yake iliyoharibika vibaya na moto ulioteketeza makazi ya watu katika Milima ya Hollywood, California.
Hii inatokea siku moja tu baada ya mtangazaji huyo wa televisheni, mwenye umri wa miaka 43, kuthibitisha kwamba aliona nyumba hiyo ikiteketea na moto moja kwa moja kupitia televisheni.
Hilton alishiriki video kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiongeza kwa uchungu kuhusiana na mshtuko mkubwa alioupata baada ya kuona nyumba yake ikiteketea kwa moto.
“Nimesimama hapa kwenye kile kilichokuwa nyumba yetu, na huzuni hii haiwezi kuelezeka. Nilipoona habari mara ya kwanza, nilikuwa katika mshtuko mkubwa sikuweza kuelewa kilichotokea. Lakini sasa, nikiwa hapa na kuona kwa macho yangu mwenyewe, nahisi kama moyo wangu umesambaratika vipande milioni moja,” ameandika Hilton
Mtangazaji huyo alinunua nyumba hiyo ya ghorofa mbili mwaka 2021 kwa dola milioni 8.4.
Idara ya Polisi ya Los Angeles (LAPD) imesema inamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kusababisha moto mkali ulioanza usiku wa kuamkia Januari 9, 2025 uliyoteketeza nyumba za kifahari zaidi ya 10,000 na kuua watu 10.
Leave a Reply