Breezy Ataka Wafungwa Waliosaidia Kuzima Moto, Wapunguziwe Vifungo

Breezy Ataka Wafungwa Waliosaidia Kuzima Moto, Wapunguziwe Vifungo

Mwanamuziki kutoka Marekani Chris Brown ameonesha kujitoa tangu kuzuka kwa moto katika milima ya Hollywood na sasa ametoa wito kwa serikali kuwapunguzia adhabu wafungwa takribani 800 kutoka CDCR waliojitokeza kupambana na moto huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Brown ameonesha kuwajali wafungwa hao huku akitoa wito wa kufanya sherehe ya kuwapongeza pamoja na kuwapunguziwa vifungo.

“Hakikisha mnafanya sherehe au paredi kwa ajili ya hawa wapambanaji waliopo mstari wa mbele na waokoaji wa kwanza baada ya haya. Pia, wafungwa waliokuwa huko wakihatarisha maisha yao wanastahili kupunguziwa muda wa vifungo vyao,” ameandika Brown

Wafungwa hao waliungana na jeshi la zimamoto jijini Los Angles kusaidia kupambana na janga hilo huku wakipokea malipo ya dola 5.80 hadi dola 10.24 kwa siku, na dola 1 kwa saa.

Mbali na hilo lakini pia rapa Brown anaamini kuwa moto ambao umeteketeza makazi ya watu na kuondoa uhai wa baadhi ya raia ni kuwa umeanzishwa na mtu na sio ukame wa kihistoria na upepo mkali kama inavyorepotiwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags