Mbunifu wa mitindo kutoka Nigeria, Liz Sanya anatajwa kukamilisha kutengeneza kiatu (sendo) kikubwa zaidi dunaini kwa kutumia masaa 72.
Kwa mujibu wa tovuti ya ‘News Center Africa’ Liz alianza mchakato wa kutengeneza kiatu hicho Januari 2 jijini Lagos huku jaribio lake la kuingia kwenye Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness (GWR) lilivutia watu wengi.
Kiatu hicho chenye rangi ya Pinki kinadaiwa kuwa na urefu wa mita 4.8 (futi 15 na inchi 9), huku akipewa motisha na wanamuziki kama Mayorkun, Pheelz, P.Priime, na Taves, pamoja na mjasiriamali wa muziki Bizzle Osikoya, Mfilimbi Korty, na wengineo,
Licha ya jitihada hizo lakini mpaka kufikia sasa Guinness World Records bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na rekodi hiyo.
Endapo mwanadada huyo ataingia kwenye kitabu cha rekodi ya dunia ataungana na mastaa wengine wenye rekodi hiyo akiwemo mpishi mashuhuri Hilda Baci, Helen Williams, Chancellor Ahaghotu na wengineo.
Leave a Reply