Filamu ya Squid Game msimu wa pili inayooneshwa kupitia Netflix imeendelea kukusanya rekodi na sasa imetajwa kuwa ndio filamu iliyofuatiliwa zaidi na watu wasiotumia lugha ya Kingereza katika jukwaa hilo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Netflix umeeleza kuwa mpaka kufikia sasa filamu hiyo imeshatazamwa na zaidi ya watu milioni 126 ndani ya siku 11 pekee.
Ikinogeshwa na mwigizaji Lee Jung-jae, msimu huo pia ulipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya pili kwenye orodha ya kila wiki na kuifanya filamu hiyo kutazamwa na watu milioni 58.2 ndani ya wiki ya mwaka mpya.
Mafanikio haya yameuweka msimu wa pili kuwa miongoni mwa mfululizo wa nne uliotazamwa zaidi duniani, ukifuatiwa na “Wednesday” pamoja na msimu wa nne wa “Stranger Things.”
Squid Game msimu wa pili iliachiwa rasmi Desemba 26, 2024 huku ikichezwa na mastaa mbalimbali wakiwemo Lee Jung-jae, Lee Byung-hun, Wi Ha-jun, Gong Yoo na wengineo.
Leave a Reply