Mshukiwa Wa Mauaji Ya Tupac Aomba Afutiwe Mashitaka

Mshukiwa Wa Mauaji Ya Tupac Aomba Afutiwe Mashitaka

Duane “Keefe D” Davis, ambaye ni mshukiwa namba moja wa mauaji ya mwanamuziki wa Hip-Hop Tupac Shakur, ameanza mchakato wa kufutiwa mashtaka dhidi yake akida kucheleweshwa kwa mchakato wa kisheria katika kesi yake.

Kwa mujibu wa ABC News, mapema wiki hii wakili wa Davis, Carl E.G. Arnold, aliwasilisha ombi la kufuta mashtaka dhidi ya mteja wake, akiamini kwamba kusubiri kwa muda mrefu kwa tarehe ya kesi kumevunja haki za kikatiba za mteja wake.

Arnold anadai kwamba kucheleweshwa kwa mashauri hayo kumesababishwa na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha pamoja na baadhi ya mashahidi kufariki hivyo sio haki kwa mteja wake kuendelea kusalia gerezani humo.

Aidha kikao cha kusikiliza ombi la Davis la kufuta mashtaka hayo kimepangwa kufanyika Januari 21 na endapo ombi hilo litakataliwa, kesi dhidi ya Davis, ambayo imepangwa kuanza kusikilizwa Machi 17 mwaka huu, itaendelea.

Davis alikamatwa huko Las Vegas mwaka 2023 kwa madai ya kuhusika kwake katika shambulio la risasi la mwaka 1996 lililofanywa kutoka ndani ya gari, ambalo lilipelekea kifo cha rapa Shakur siku chache baadaye.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags